NADIR 'CANNAVARO' ASTAAFU STARS

BEKI  wa kati wa timu ya soka ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’  (pichani) ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa  'Taifa Stars'.
 Hivi karibuni Cannavaro ambaye pia ni nahodha msaidizi wa Stars hakuitwa kwenye kikosi cha kocha Jan Poulsen kinachojiandaa na mechi ya kutafuta kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2014) dhidi ya Msumbiji itakayopigwa Februari 29 kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
 Nyota huyo alisema amefikia uamuzi huo ili kuwapa nafasi na wengine kuitumikia timu hiyo na kuendelea kuwekeza nguvu zaidi katika klabu yake ya Yanga, huku akiatarajia  kuandika barua kwa   Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulitaarifu juu ya uamuzi wake.
 

Comments