MWAPE AWAPA RAHA YANGA SC

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Davies Mwape amezipamba sherehe za miaka 77 za timu hiyo kwa kufunga bao pekee walipoilaza Ruvu Shooting 1-0 jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Ushindi huo umewafanya mabingwa hao watetezi Yanga kufikisha pointi 37 na kurudi kileleni na Simba iliyoichapa Azam 2-0 imeshuka nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao.Mshambuliaji Mwape aliipatia Yanga bao hilo pekee katika dakika ya 46 kwa shuti kali baada ya kuunasa mpira uliokolewa vibaya na beki wa Shooting, Idd Nyambiso mwanzoni mwa kipindi cha pili.Matokeo hayo yameifanya Yanga kujiweka vizuri kabla ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zamalek ya Misri utakofanyika mwishoni mwa wiki hii.

Comments