MUSTAFA HASSANALI KUONYESHA UBINIFU WAKE NIGERIA



MBUNIFU maarufu wa mitindo nchini Mustafa Hassanali, anatarajiwa kuwa miongoni wabunifu wa mitindo 77 kutoka mabara 6 duniani watakaoshiriki katika maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ARISE Magazine Fashion Week(AMFW) yanayotarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria mwezi ujao.
Hassanali alisema mualiko huo ni sehemu nyingine ya mafanikio yake aliyoyaonesha katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikishika kasi siku hadi siku.
Alisema ushiriki wake pia utakuwa na faida kubwa sana katika kazi zake za ubunifu kutokana na ukwelki kwamba utamuwzesha kukutana na wambunifu wengi kwa wakati mmoja hivyo kuweza kubadilishana ujuzi na mawazo.
Hassanal;I alisema maonyesho hayo yatafanyikia katika viwanja vya hoteli maarufu na ya kifahari ya Federal Palace Hotel ya jijini Lagos kuanzia Machi 6 hadhi 11 Machi ambapo mamia ya wadau wa tasnia hiyo watapa fursa ya kushuhudia kazi za wambunifu hao.

Comments