MTOTO WA WHITNEY AKUTWA AKIBWIA UNGA MASAA MACHACHE BAADA YA MAMA YAKE KUZIKWA


NEW JERSEY, Marekani
MTOTO wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown anadaiwa kufumwa akivuta madawa masaa machache tu baada ya mazishi ya mama yake.

Inadaiwa masaa manne  hivi  baada ya shughuli za mazishi kumalizika Bobbi Kristina (18) akiwa na marafiki zake pamoja na ndugu ghafla alitoweka na kwenda kusikojulikana.

Ingawaje mtu wa karibu na familia ya Houston alisema Kristina alipelekwa kwenye kituo cha mafunzo ya kuacha dawa za kulevya mwaka jana.

Binti huyo amekuwa huku akimuona mama yake akitumia dawa za kulevya, familia yake imekuwa na wasiwasi mkubwa wa Kristina kufuata nyayo za mama yake. 

Comments