KIYOVU KUTUA KESHO TAYARI KUKABILI SIMBA J'2


MSAFARA wa watu 25 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu ya Kiyovu ya Rwanda unatarajiwa kuwasili kesho tayari kwa mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba itakayopigwa Jumapili katika dimba la Taifa.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema  kitafikia katika Hotel ya Wanyama iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
 Alisema kikosi cha Simba  kipo kambini Bamba Beach kikiendelea kujifua na mchezo huo ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokuwa Juma Jabu na Ulimboka Mwakingwe.
Aidha, beki wa timu hiyo Victor Costa ambaye alikuywa anakabiliwa na malaria ameshapona na jana aliripoti katika kambi ya timu hiyo.


Comments