MICHAEL WAMBURA AWASILISHA PINGAMIZI LA UCHAGUZI DRFA


MICHAEL WAMBURA
                              

February 7, 2012

MWENYEKITI,

KAMATI YA UCHAGUZI ,

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


YAH: KUSIMAMISHA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA DAR-ES-SALAAM(DRFA) ULIOPANGWA KUFANYIKA 18/3/2012



MR MICHAEL RICHARD WAMBURA (Mlalamikaji), nimelazimika kuleta maombi na malalamiko yangu mbele yako na kamati yako kuhusiana na uchaguzi tajwa hapo juu wa DRFA kutokana na uvunjifu wa kanuni, maagizo na Katiba ya TFF sambamba na katiba ya DRFA na sheria za nchi katika mchakato mzima wa kuelekea katika uchaguzi huo kama ifuatavyo.

1. Uundwaji wa kamati ya chaguzi ya DRFA umevunja kanuni ya uchaguzi wa wanachama wa TFF (TFF MEMEBERS STANDARD ELECTROL CODE) Ibara ya 3(2) inakataza mtu mmoja kuwa mjumbe wa kamati mbili za uchaguzi za wanachama wa TFF au wanachama washiriki wa TFF “The members of the Committee shall under no circumstances be member of the executive body of TFF or Executive body of the Association or Executive of other TFF member Association or the Elections Committee of the other member association of TFF or Executive body /Elections Committee of a subordinate” kwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Muidin Ndolanga Pia Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya FRAT(taifa ambao wote ni wanachama wa TFF basi uhalali wake wa kuwa m/kiti wa kamati ya Uchaguzi wa DRFA unakuwa haupo kwa kuwa unavunja kanuni za uchaguzi , aidha Nd Damas Ndumbaro ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Simba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na katibu wa Kamati ya uchaguzi wa FRAT, anapoteza sifa za kuwa Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya DRFA, kwa maana hiyo naomba tamko la kuwa mchakato mzima wa uchaguzi ufutwe na kuanza upya kwa kuwa haukufuata taratibu na kanuni husika .

2. Katiba ya DRFA toleo la 2008 ibara ya 1(6) inatamka kuwa “DRFA itaheshimu Katiba, Kanuni Maagizo na Maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake” TFF kupitia barua yake kumbukumbu TFF/ADM/EC/36 ya tarehe 22/7/2011 yenye kichwa cha habari “ Katiba za Wanachama na Wanachama wao” kwenda kwa makatibu ambapo iliagiza kufanyika mabadiliko katiba zao ili ziendane kikamilifu na katiba ya mfano ya TFF aidha TFF kupitia barua yake ya tarehe 12/12/2012 yenye kumbukumbu TFF/TECH?GC11/115 kwenda kwa makatibu wa wilaya ikikumbushia kurekebisha katiba zao ili ziendane na Katiba ya mfano ya TFF, Kwa kuwa Katiba za wanachama wa DRFA na DRFA hazijafanyiwa marekebisho na wahusika ni wazi hawajatekeleza maagizo ya TFF hivyo kwenda kinyume na Katiba ya TFF 12(d)(e) & (n) na Ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi za TFF na Wanachama wake.

3. Kwa kuwa wilaya wanachama wa DRFA hawakufuata kanani za Uchaguzi za TFF na Wanachama wake, kumepelekea baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutokuwa na sifa ikiwemo ya Elimu isiyopungua kidato cha Nne ikiambatana na Cheti cha Matokeo kama ilivyoagizwa na TFF katika barua yake kwa wanachama wake na wilaya, kwa kuwa viongozi hao wa wilaya wanakosa sifa ya kuwa viongozi ni wazi pia wanakosa sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, itakumbukwa katika Uchaguzi wa Chama cha mpira Mkoa Mara(FAM) ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF alikuwepo ambapo Nd MAGOTI ambaye alikuwa Katibu wa Chama cha mpira Wilaya ya Bunda aliondolewa katika kugombea na hakurusiwa kupiga kura baada ya kuonekana hakuwa na sifa ya kuwa Katibu wa wilaya kutokana na tatizo la Elimu halikadhalika Katibu wa Wilay ya Serengeti Ombeni Magati nae aliondolewa katika kugombea ujumbe wa kamati ya Utendaji na pia hakuruhusiwa kupiga kura na nafasi walizokuwa wanazishikilia kutangazwa kuwa ziko wazi, hivyo ni matumaini yangu hata katika DRFA na wanachama wake mkondo utafuata huo huo.

4. Katiba ya DRFA ibara ya 30(2) inayozungumzia sifa za wagombea “Awe na kiwango cha Elimu cha kidato cha nne au inayoyolingana nayo” hivyo inakinzana na katiba ya mfano na kanuni za uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) amboyo ina tamka wazi any person contesting any position “ Must have minimum academic qualification of form Four and holder of a certificate of ordinary Secondary Education” kwa mantiki hiyo katiba hii inazua mgongano sio tu na katiba kanuni na maagizo ya TFF bali hata sheria za nch kwa katika Tanzania hakuna elimu nyingine yoyote inayofanana na ya Kidato cha Nne.

5. Katiba ya DRFA Ibara ya 30(6) “ kiongozi anaemaliza muda wake atakuwa na haki ya kutetea nafasi yake ili mradi awe na afya njema na akili timamu” ibara hii inaukinzani mkubwa na kanuni katiba na maelekezo ya TFF, aidha kanuni hii inatoa taswira ya kuwa kiongozi anaye maliza muda wake hapaswi kuwa na sifa za Msingi kama zilivyo ainaishwa kwenye kanuni za uchaguzi za TFF na wanachama wake Ibara ya 9, aidha , ibara hii inalenga kumruhusu hata mtu aliyeingia madarakani kimakosa kuendelea kugombea nafasi aliyoipata kimakosa hata baada ya kugundua makosa kwa kuwa tu ndie anayemaliza muda wake hivyo ana haki ya kugombea, kipengele hicho kingekuwa na maana kama kingemruhusu mgombea ili mradi awe na sifa za msingi za kugombea.itakumbukwa kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Mzee Hasan Dalali aliondolewa kugombea kwa sababu ya kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne huku Mwenykiti wa sasa wa DRFA ndugu Amin (AKA Bakhresa) na Nd Damas Ndumbaru wakiwa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyotekeleza na kuzingatia Kanuni za uchaguzi za TFF, aidha Nd A. Bulembo nae aliondolewa kwa vigezo hivyo hivyo katika uchaguzi wa timu Villa Squad ya DSM, kanuni haikuishia hapo iliendelea mpaka kwa timu ya Coastal Union ya Tanga, kwa misingi hiyo ni wazi kamati hii haitafumbia macho kwenye hili la DRFA.

Kwa kuzingatia Maelozo hayo hapo, Ninawasilisha katika maombi ya dharura kama ifuatavyo:


(a) Tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ivunjwe na kuundwa upya.

(b) Tamko kuwa Mchakato mzima wa uchaguzi uanze upya mara baada ya Kamati mpya kuundwa.

(c) Tamko katiba ya DRFA ina kinzana na katiba Kanuni na Maelekezo ya TFF hivyo ifanyiwe marekebisho. yanayostahili kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.

(d) Tamko la kufanyika kwa Uhakiki wa sifa za viongozi wa wanachama na wanachama washiriki wa DRFA ili kuridhia matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba za Mfano za wiliya zilizotolewa na TFF.

Comments

Post a Comment