MATT HARDY KUFANYIWA UPASUAJI


MBABE wa mieleka Matt Hardy anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa bega lake alilowahi kufanyiwa miaka mitatu iliyopita.
Matt Hardy aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na moja ya mtandao wa People.com alisema anatarajia kufanyiwa upasuaji huo ambao aliwahi kufanyiwa miaka mitatu iliyopita baada ya kuumizwa na mbabe The Undertaker.
Alisema "kwangu sikufikiria kama bega hili lingeweza kunisumbua kwa muda mrefu kama hivi ilivyo na kufikia daktari kuniambia nahitaji kufanyiwa upasuaji mwingine. Lakini pia najilaumu kwa kuamua kucheza na mbabe huyo ambaye niliamini kama ningefanikiwa kumchapa ningepata umaarufu zaidi ila cha kushangaza nimejikuta nikiambulia kuumia bega”.




Comments