MANCHESTER ZOTE KAZINI ULAYA LEO

WAWAKILISHI wa England katika michuano ya Europa League, Manchester United na Manchester City, ndizo zimeteka hisia za michuano hiyo hatua ya 16 bora, ambayo inaanza leo.
Kwa sasa Manchester United, ambao ni mabingwa wa England, wanachuana na Manchester City katika kuwania ubingwa wa msimu huu wa ligi hiyo, pia wanapewa nafasi kubwa ya kukutana kwenye fainali ya Europa League.
United watacheza na Ajax ya Uholanzi, mechi ya kwanza ikipigwa leo mjini Amsterdam.
City, ambayo inaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi mbili zaidi ya wapinzani wao hao, watamenyana na mabingwa watetezi wa Europa League, FC Porto ya Ureno, wakati mechi nyingine kali inatarajiwa kuwa kati ya Lazio na Atletico Madrid.
United ndiyo timu kubwa zaidi kucheza Europa League miaka ya karibuni na kocha Alex Ferguson bado haamini kama timu yake ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa na FC Basel ya Uswisi.
“Yalikuwa matokeo ya kustaajabisha mno ambayo sikuamini, kwa sababu hisia zangu ni kwamba kama tungevuka, tungefika fainali,” alisema Ferguson.
Kocha huyo Mscotland amepuuza tetesi kwamba hatayatilia uzito mashindano.
Europa League, zamani ikiitwa UEFA Cup, ni moja kati ya mataji ambayo Ferguson hajatwaa.
“Nayachukulia kwa uzito mashindano haya,” alisema. “Kitu kikubwa kuhusu Alhamisi ni kwamba hatuna mechi Jumamosi ijayo, hivyo nitachezesha kikosi changu kamili,” alisema.
Stoke itakuwa nyumbani kuikaribisha Valencia, wakati Sporting watakuwa Legia Warsaw.
Udinese itakuwa mwenyeji wa PAOK ya Ugiriki, PSV Eindhoven itaifuata Trabzonspor.

RATIBA KAMILI UEFA NDOGO LEO:
Lokomotiv Moscow v Athletic Bilbao (saa 2:00 usiku)
Rubin Kazan v Olympiacos (saa 2:00 usiku)
AZ v Anderlecht (saa 3:00 usiku)
Lazio v Atletico Madrid (saa 3:00 usiku)
SV Red Bull Salzburg v FC Metalist (saa 3:00 usiku)
Ajax v Man Utd (saa 3:00 usiku)
Plzen v Schalke 04 (saa 3:00 usiku)
Legia Warsaw v Sporting Polish (saa 3:00 usiku)
Wisla Krakow v Standard Liege (saa 5:05 usiku)
Udinese v PAOK Salonika (saa 5:05 usiku)
Trabzonspor v PSV H. Avni (saa 5:05 usiku)
Hannover 96 v Club Brugge (saa 5:05 usiku)
FC Porto v Man City (saa 5:05 usiku)
Stoke v Valencia (saa 5:05 usiku)
Steaua Bucuresti v FC Twente (saa 5:05 usiku)

Comments