Kikosi cha Mambas
Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas)
itawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya South African
Airways. Ndege hiyo yenye mruko namba SA 186 inatarajia kutua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.55 mchana.
Msafara wa Mambas kwa ajili
ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano (Februari 29 mwaka huu) saa
10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa na watu 29. Kati
ya hao, 19 ni wachezaji wakati waliobaki ni maofisa wa timu hiyo.
Mwamuzi wa mechi hiyo Farouk
Mohamed na wasaidizi wake Ayman Degaish, B.T Abo El Sadat na Gihed Greisha
kutoka Misri watawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya Egypt
Air. Kamishna ni Loed Mc Ian kutoka Afrika Kusini.
Tiketi kwa ajili ya mechi
hiyo zitaanza kuuzwa Jumanne (Februari 28 mwaka huu) katika vituo vya vya Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi
(Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta
cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments
Post a Comment