MAKOCHA WAZUNGUMZIA MPAMBANO WA KESHO UWANJA WA TAIFA

Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Taifa Stars Jan Paulsen akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliok,utanisha kocha huyo pamoja na wa timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika ofisi za TFF jijini Dar es salaam leo, wakati makocha hao walipozungumzia maandalizi ya mpambano wa kesho kati ya timu hizo ambapo amesema anaamini kwamba mchezo huo utakuwa ni sehemu nzuri ya mazoezi kabla ya kikozi chake kukutana na Msumbiji.


 
Naye kocha wa DRC Muntubile Santos wa pili kutoka kulia amesema anaifahamu Tanzania na anaiheshimu, lakini pia aliamua kuichagua Tanzania kutokana na soka lake linalofanana na soka la Kiingereza hivyo anaamini kwamba mpambanbo huo utakuwa ni mazoezi mazuri kabla ya kukutana na timu ya Sychelies. Wengine katika picha kutoka kushotoBoniface Wambura Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na Nzila Fanan afisa habari wa shirikisho la mpira wa miguu nchini DRC Congo na.

Comments