Kiingilio kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya
kimataifa kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
itakayofanyika Februari 23 mwaka huu kitakuwa sh. 2,000 kwa viti vya kijani na
bluu.
Mechi itachezwa kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam ambapo viti hivyo vya kijani na bluu vinachukua
watazamaji 36,693 ambayo ni karibu theluthi mbili ya viti vyote kwenye uwanja
huo wa kisasa.
Viti vya rangi ya chungwa
kiingilio ni sh. 5,000, VIP C itakuwa sh. 7,000 wakati VIP B tiketi zitauzwa kwa
sh. 10,000. Kiingilio kwa viti vya VIP A kitakuwa sh. 15,000.
Kwa vile Februari 23 mwaka huu ni siku ya
kazi ili kutoa fursa kwa washabiki wengi kushuhudia pambano hilo la kimataifa,
mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni.
Wakati Taifa Stars
inayofundishwa na Jan Poulsen imeingia kambini leo na ikitarajiwa kuanza mazoezi
jioni kwenye Uwanja wa Karume, DRC ambayo iko chini ya kocha Claude Le Roy
inatarajia kutua nchini kesho.
Taifa Stars na DRC zinatumia
mechi hiyo kunoa wachezaji wao kabla ya mechi zao za mchujo za Kombe la mataifa
ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Katika raundi hiyo ya awali
ambayo mechi zake zitachezwa Februari 29 mwaka huu, Stars itaanzia nyumbani
dhidi ya Msumbiji wakati DRC inaanzia ugenini dhidi ya Seychelles.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments
Post a Comment