KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka  Tanzania  (TFF) Angetile Osiah (pichani) anatarajia kufanyiwa upasuaji wa kichwa nchini India wiki ijayo.
 Angetile ambaye alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili  katika wodi ya taasisi ya Mifupa (MOI)kabla ya kuruhusiwa jana amesema kuwa upasuaji huo unafuatia matokeo ya vipimo na ushauri toka kwa madaktari.

Comments