HAYA NDIYO YALIYOMKUTA BOBBY BROWN KWENYE MSIBA WA WHITNEY

MAZISHI ya mwanamuziki nyota duniani, Whitney Houston yalifanyika katika ukumbi wa kanisa la New Hope Baptist, Newark jana, lakini ajabu mtu mmoja tu muhimu ambaye hakuonekana ni mume wake wa zamani, Bobby Brown.
Mashahidi waliiambia Us Weekly kwamba Brown; “Aliruhusiwa kuingia ndani, kutoa heshima zake za mwisho na kisha kuondoka. Macho yake yalikuwa ya njano, akaenda kwenye jeneza kisha na kuondoka. Alikuwa pale kwa dakika 15”.
Kuhusu tetesi kwamba alifukuzwa na uvumi kwamba hakuonekana kabisa, Brown, ambaye alitarajiwa kutumbuiza kwenye shoo yake moja jana, ametoa taarifa rasmi akizungumzia sakata zima.
“Mimi na watoto wangu tulikaribishwa kwenye mazishi ya mke wangu wa zamani Whitney Houston. Tuliketi chini ya ulinzi mkali na baadaye tukaamriwa kuondoka kwa njia tatu tofauti. Nilishindwa kuelewa kwa nini walinzi waliifanyia hivi familia yangu na kuendelea kutuuliza, hakuna mwingine pia wa kuondoka. Walinzi pia walinizuia kwenda kumuona binti yangu Bobbi Kristina (aliyezaa na Whitney).
Katika mwanga kwenye msiba huo, nikapiga busu jeneza la mke wangu wa zamani na kuondoka kinyonge. Watoto wangu waliboreka kabisa na tukio hili. Hii ilikuwa siku ya kumpa heshima Whitney. Nina shaka kama Whitney alitaka haya. Nitaendelea kumuenzi mke wangu wa zamani katika njia nzuri ninayoijua,” alisema Bobby.
Mapema wiki hii, chanzo kilisema kwamba hakuna uhusiano mzuri baina ya ndugu za Houston na Brown, aliyemuoa Houston mwaka 1992, kabla ya kuachana rasmi mwaka 2007.
“Kuna wana familia wanaofikiri Bobby alimfanya Whitney aingie kwenye dimbwi la kutumia dawa za kulevya,” chanzo kimoja kilisema. “Lakini sasa Bobby ni msafi na Whitney kwa bahati mbaya amefariki dunia. Hivyo, kuna chuki,”.

Comments