Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na
Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar
es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana
na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa
mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi
(kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.
(Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Mkurugenzi
wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara
baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki
uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lisu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili
uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi
(Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia).
Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lisu
Mbunge wa
Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media
Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya
kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi
wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel
Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu..
Comments
Post a Comment