HAPA CHEGE&TEMBA, PALE AY&FA NI NDANI YA DAR ALIVE J'2 HII




Na Mwandishi Wetu

WIKI moja baada ya kukamilisha shoo ya ukweli iliyowahusisha Juma
Nature na Nameless, kesho Jumapili ndani ya Dar Live kutakuwa na mzigo
mwingine wa ukweli utakaowahusisha AY na MwanaFA wakionyeshana ubabe
na Chegge na Temba.
Mratibu wa Burudani wa Dar Live, Juma Mbizo ameweka wazi kuwa baada ya
kufanikiwa katika shoo iliyopita, timu yake imejiandaa kupokea idadi
kubwa ya mashabiki, huku akisisitiza kuwa wasanii watakaotoa shoo siku
hiyo wote wameshakamilisha maandalizi.
“Kinachongojewa ni muda tu ili kukamilisha shoo hiyo, wasanii hao wote
hawahitaji kuelezewa juu ya ubora wao, wakazi wa Dar na vitongoji
vyake wanakaribishwa kuona mapinduzi ya burudani,” alisema Mbizo.
Burudani ya siku hiyo itakuwa imesheheni zaidi kwa makundi maarufu ya
taarabu ya East African Melody chini ya mkongwe Mwanahawa Ally na TOT
Taarab inayoongozwa na Khadija Kopa yatakapoonyesha kazi.
Kwa upande wa dansi wakali wa miondoko hiyo African Stars International ‘Twanga Pepeta’ wataonyesha vitu vyao.
Aidha, aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mchujo wa washiriki 30
wa Shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna ambao wataanza kushiriki shindano hilo hatua ya mchujo kwa mara ya kwanza.
Kinadada watakaoonyeshana kazi ni katika vaa, imba na cheza kama
Rihanna ni: Aisha Hassan, Wellu Sengo, Fatna Kivava, Nitaedith Richard, Babro Beckerham, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’, Hellen David,
Pasilida Mandari, Doroth Remi, Blandina Godfrey, Lailath Mohamed,
Maria Christopher, Raya Ally, Elifuraha Ephraim, Caroline David,
Pamela Daffa na Rozina Jonas.
Wengine ni Rukia Mohamed, Like Abraham, Zaitun Yahaya, Anatolia Raphael, Asia Halfan, Anna Maya, Lydia Masisi, Lilian Pissy, Neema Abraham, Rachel Jailos, Suleiya Abdallah na Evelyne Leonard.

Comments