FAINALI KUCHELEWA KUANZA AFCON 2012

MUDA wa kuanza kwa mchezo wa fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumapili utachelewa kuanza kwa nusu saaa kutokana na "matatizo ya kiufundi". Mchezo wa fainali kati ya Zambia na Ivory Coast utakaochezwa mjini Libreville, uliokuwa uanze saa nne usiku saa za Afrika Mashariki, sasa utaanza nusu saa baadaye- saa nne na nusu usiku.Shirikisho la Soka Barani Afrika Caf, halijatoa sababu yoyote zaidi kuhusiana na mabadiliko hayo.Tiketi za mchezo wa fainali hazijafanikiwa kuuzwa zote kama ilivyotarajiwa, huku robo tatu ya tiketi hizo zikiwa hazijanunuliwa.Waandaaji wamesema siku ya Jumatano kuwa asilimia 70 ya tiketi, zimeuzwa kwa ajili ya mchezo huo katika mji mkuu wa Gabon siku ya Jumapili.Zambia itacheza mechi ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya tatu kwenye uwanja wa de l'Amitie, wakiwa wanatafuta kunyakua kombe la Afrika kwa mara ya kwanza.Ivory Coast itakuwa ikitafuta ushindi kwa mara ya pili, miaka 20, baada ya kucheza na kushinda mechi ya fainali dhidi Ghana.Timu hizo mbili zinakutana baada ya Chipolopolo kutoka Zambia kuichapa Ghana 1-0 mjini Bata, huku Ivory Coast wakiichapa Mali 1-0 mjini Libreville siku ya Jumatano.

Comments