DALGLISH UTAMTAKA KWA FURAHA YAKE

KOCHA wa Liverpool, Kenny Dalglish ameiambia BBC Sport kwenye Uwanja wa Wembley kuwa ubingwa wa Kombe la Ligi ndiyo mwanzo wa kuleta vikombe kwenye Uwanja wa Anfield.
'The Reds' ilibidi kusubiri mikwaju ya penalti kutwaa ubingwa na Dalglish anaamini kuwa kutwaa ubingwa ni kutokana na morari na ya wachezaji. "Licha ya kuwa tumetwaa ubingwa leo, huo si mwisho," alisema kocha huyo mwenye miaka 60 baada ya klabu yake kumaliza ukame wa vikombe wa miaka sita.
"Hatutaki kuishia hapa, Tunataka kuendelea. Tumeshinda na tunafurahi kufanya hivyo. Nafahamu jinsi gani wachezaji walivyofuahia ushindi na kila mmoja anaendelea kufurahi."
Aliisifu Cardiff kuwa kuipa Liverpool changamoto lakini akasema kuwa yote kwa yote timu yake ilikuw aikistahili ushindi."Tangu mwanzo, wakati tunacheza na Exeter City katika raundi ya pili, tyulisema kuwa tunaingia kwenye mashindano tukiwa makini, hatukutaka mchezo," alisema Dalglish.

Comments