CHONDE CHONDE WATANZANIA TUKAISHANGILIE YANGA JUMAMOSI:PROF.JAY


MSANII wa muziki wa bongo fleva nchini  Joseph Haule  'Prof J', amewataka Watanzania kuweka utaifa mbele kwa kuishangilia Yanga katika mchezo wake na Zamelek utakaopigwa Februari 18 mwaka huu.
J alisema siku hiyo Watanzania  wanapaswa kujitokeza kwa wingi huku wakiungana kwa pamoja kutoa sapoti kwa wachezaji wa Yanga kwa kuwa wanaiwakilisha Taifa.
“Mimi mmoja wa mashabiki wa Simba lakini siku hiyo nitatoa sapoti kwa timu ya nyumbani  Yanga kwani utaifa ni muhimu kuliko kitu kingine”alisema Prof J
Prof. J alisema kwa kufanya hivyo itakuwa ni hatua moja mbele katika  kufanya mapinduzi ya maendeleo ya mchezo huo unaopendwa na wengi hapa nchini.
Alisema ushabiki wa kuzizomea timu za hapa nyumbani zinapocheza na wageni hausaidii kuinua kiwango cha soka na kuliletea Taifa mafanikio bali unazindi kurudisha nyuma mafanikio yanayotarajiwa.
Prof J alisema Watanzania ni muhimu wakaweka utaifa mbele kwa kuzishangilia timu zao kwa kuwa kila timu inaposhinda ni taifa ndilo linalopata heshima na kutambulika katika mchezo huo duniani.

Comments