BHINDA AKANA KUCHACHUA MAPATO YA YANGA, ZAMALEK


MJUMBE wa kamati ya utendani ya klabu ya soka ya Yanga, Mohammed Bhinda (Pichani) amekana kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mapato ya mechi ya Ligi ya mabingwa Afrika baina ya Yanga na Zamalek uliofanyika jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Aidha, Bhinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya klabu ya Yanga amekana kuwa hajasimamishwa uongozi ndani ya klabu hiyo kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hivi karibuni.
 Bhinda alisema anashangazwa na taarifa hizo zisizo na ukweli wowote ambazo anaamini zinalengo la kumchafua yeye, klabu ya Yanga pamoja na Wanayanga kwa ujumla.
Alisema kuwa, siku chache kabla ya timu hizo kuvaana mkurugenzi wa Primetime Promotion ambao walikuwa wanaratibu mechi hiyo, Joseph Kusaga ambaye alimuomba amsaidie kuuza tikeki za mchezo huo katika maeneo ambayo ni sumbufu ambapo alikubali na kuingia mkataba kama Bhinda na si mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.
“Sikuona haja ya kumkatalia kwa sababu uongozi ulinipa jukumu la kushirikiana nao kwa namna moja ama nyingine, hivyo nilitafuta baadhi ya wanachama waaminuifu wa Yanga na kuwapa kazi hiyo ambayo waliifanya kwa uadilifu mkubwa na mwisho wa siku zilipatikana shilingi mil.71,544,000,”Alisema.
Bhinda aliongeza kuwa baada ya makabidhiano ya pesa hizo na tiketi zilizobaki aliomba kurudishiwa fedha zake ambazo alitumia katika kuwalipa posho maofisa wa polisi, wakata tiketi na usafiri ambapo alirejeshewa, huku Kusaga akimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na hasa ikizingatiwa kuwa vituo alivyopewa huwa vina usumbufyu mkubwa.
“Sina matizo na Primetime Promtions, hata wanayanga niliowapa kazi hiyo l;akini nashangaa taarifa hizo zinatoka wapi,napenda kuwaondoa wasiwasi wanayanga wenzangu kuwa mimi bado mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga, sijasimamishwa  na nitaendelea kuwa mwanachma wa Yanga,”alisema Bhinda.

Comments