MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi alitupia mabao manne
nyavuni na kufikisha mabao 40 kwa msimu wa tatu mfululizo, huku akiiwezesha Barcelona
kushinda 5-1 dhidi ya Valencia jana.
Barcelona ilitoka nyuma na kupunguza deni la pointi hadi
kubaki 10 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Real Madrid, ambao Jumamosi waliifunga Racing
Santander 4-0.
Muuwaji alikuwa Messi, ambaye akicheza mechi yake ya 200 ya
La Liga alikutana na kipa ‘mnyela’ Diego Alves aliyemfanya afikishe mabao 27
kwenye La Liga msimu huu na 42 kwenye
mashindano yote na kwa jumla 146 katika mechi zote za ligi, akiwa na Barcelona.
“Timu ilicheza mchezo wa kuvutia,” alisema Messi, ambaye
mabao mengine manne aliyowahi kufunga katika mechi moja ilikuwa dhidi ya Arsenal
kwenye Ligi ya Mabingwa miaka miwili iliyopita.
Pablo Piatti aliifungia Valencia dakika ya tisa bao la kuongoza
na Xavi Hernandez akaisawazishia Barcelona.
Mapema, Athletic Bilbao ilifunga mabao matatu katika dakika
nne za mwisho za kipindi cha pili na kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Malaga,
wakati Levante ilipigwa 5-3 na Rayo Vallecano.
Katika mechi nyingine ya La Liga jana, Ikechukwu Uche alipiga
mabao mawili Granada ikiwafunga 4-2 Real Sociedad waliocheza pungufu ya
mchezaji mmoja na Mallorca ikashinda 4-0 dhidi ya Villarreal.
Comments
Post a Comment