AZAM FC WAIONYA SIMBA SC

AZAM FC kupitia kwa kocha wake msaidizi Kalimangonga Ongala (aliyeinua mkono)amesema kwamba hawaihofii Simba pamoja na ukubwa iliyonayo hivyo ameitaka isubiri kipigo kitakatifu katika mechi yao ya ligi kuuu soka Tanxania bara itakayopigwa kesho kwenye dimba la Taifa.
Ongala amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwamba timu yake ipo vizuri na imejipanga kushinda mechi zote zilizobaki katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
"Kikosi changu kipo vizuri na tumejipanga kushinda michezo yote iliyosalia katika duru hili la mwisho hivyo Simba nao ni lazima wakumbane na kipigo hicho, "Alisema.

Comments