AZAM FC RUKSA KUMTUMIA KIPRE BALOU

Mshambuliaji Kipre Bolou Wilfried aliyejiunga na Azam kutoka Ivory Coast sasa ni ruksa kuichezea timu hiyo michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF) jana (Februari 9 mwaka huu) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji huyo aliyeombewa uhamisho katika dirisha dogo la usajili kutoka timu ya Sewe Sport ya nchini humo.

Comments