ARUSHA WATAMBA KUCHUKUA MEDALI ZOTE KILI MARATHON 2012

 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia nikocha wa riadha wa timu ya mkoa wa Arusha, John Bayo (kushoto) akizungumzajambo na wanariadha wanaouwakilisha mkoa wa Arusha katika Mashindano ya mwakahuu ya Kilimanjaro Marathon yatakayofanyika kesho mjini Moshi. Kulia ni MenejaMasoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu hiyo kushiriki mashindanohayo
 Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timuya Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012, akiwapamkono wa heri na kuwatakia ushindi wanariadha hao 18, wanaouwakilisha mkoa waArusha katika mbio hizo zitakazofanyika kesho mjini Moshi, mkoani Kilimnajaro.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia ni kochawa riadha wa timu hiyo, John Bayo.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minjawalioidhamini timu ya Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za KilimanjaroMarathon 2012, akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha.

 Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minjawalioidhamini timu ya Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za KilimanjaroMarathon 2012, akiwa katika picha ya pamoja na makocha wanaoinoa timu ya mkoawa Arusha
 Wachezaji wa timu ya Riadha ya mkoa wa Arusha inayoshirikimashindano ya Kilimanjaroo Marathon 2012 wakijiandikisha kushiriki mashinadohayo jana tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayofanyikia kesho mjini Moshimkoani Kilimajaro. Timu hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijiniDar es Salaam na inajumla ya wakimbiaji 18
 Wachezaji wa timu ya Riadha ya mkoa wa Arusha inayoshirikimashindano ya Kilimanjaroo Marathon 2012 wakijiandikisha kushiriki mashinadohayo jana tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayofanyikia kesho mjini Moshimkoani Kilimajaro. Timu hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijiniDar es Salaam na inajumla ya wakimbiaji 18

Na Mroki Mroki,Moshi
TIMU ya riadha kutoka Mkoa wa Arusha, imejigamba kuibuka naushindi mnono katika Mshindano ya mwaka huu ya mbiuo za nyika yajulikanayo kama Kilimanjaro Marathon 2012 yatakayofanyika kesho mjiniMoshi mkoani Kilimanjaro.
 Timu hiyo ambayo, imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors yajijini Dar es Salaam imesema mwaka huu haipotayari kuachia medali za dhahabu, Shabana fedha ziende nchini Kenyana badala yake watahakikisha kuwa zinabaki hapa nchini. 
“Tumejipanga vizuri sana mwaka huu na wachezaji wetu wotewaliingia kambini kujifua vizuri chini ya udhamini mzuri wa CFAO Motors, hivyowatanzania wake tayari kushangilia ushindi”,alisema Kocha wa timu hiyo ambayepia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha,John Bayo. 
Aidha Bayo alisema timu ya Arusha inaundwa na wachezajimashuhuri na walio na rekodi nzuri za mashindano hayo nay ale ya kimataifa. 
 Aliwataja wachezaji wanounda timu hiyo ya Arusha iliyo nawakimbiaji 18 kuwa ni Fabiola William, Banuuelia Katesigwa, Flora Kagali,Rebeca Kavina, Daudi Joseph, Mashaka Masumbo, Yohana Masuka na Josepha Eliasambao hukimbia Full Marathon. 
Wengine watakao kimbia Nusu marathon (21km) ni Mary Naali,Fabian Joseph, Faustine Mussa, Ezekiel Jfari, Uwezo Lukinga, Rogart John,Joseph Francis, Restituta Joseph, Jacquline Sakilu na Damian Chopa.  
Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO iliyodhamini timu hiyoya mkoa wa Arusha, Alfred Minja, amesema kampuni yake imetumia Shilingi milioni35 katika mashiondano ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kudhamini timu hiyo nauratimu waa mashindano. 
Minja alisema mwaka wa 10 sasa CFAO Motors inadhaminimashindano ya Kilimanjaro Marathon na mwaka 4 sasa kudhamini timu ambazozimekuwa zikifanya vizuri. 
Aidha amesema CFAO Motors itakuwa na meza maalum ya kugawamaji, soda, vitafunwa na burudani ya muziki kwa katika eneo la Mweka ambapowakimbiaji watakuwa wakigeuzia. 
Minja amesema CFAO Motors, mbali na kudhamini wachezaji haowa timu ya Arusha 18 lakini pia inawakimbiaji wengine 25 wa nusu marathonkutoka jijini Dar es Salaam. 
Mashindano ya Mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yanatarajikuwa na shamra shamra za aina yake Ambatopia yatakiwa yanatimiza mwaka wa kumi tangu kuanza kufanyika.

Comments