AMIR MAFTAH AUMIA TENA

WIKI moja tu baada ya kurejea dimbani kwa beki wa kushoto wa klabu ya soka ya Simba Amir Maftah (pichani), hali imekuwa si shwari tena baada ya beki huyo kuumia mguu katika mazoezi ya timu hiyo jana.
Awali Maftah alikuwa nje kwa miezi kadhaa kutokana na kuwa majeruhi kabla ya kupona na hatimaye kucheza mechi mbili za timu hiyo kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.
Daktari wa Simba Cosmas Kapinga alisema jana kwamba maumivu hayo yatamfanya Maftah kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki mbili.

Comments