YANGA YAPELEKA DIGIDIGI ZENJI

WAKATI michuano ya soka ya kombe la Mapinduzi ikianza jana Visiwani Zanzibar, mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara  Yanga, wanadaiwa kupeleka wachezaji wengi wa kikosi cha pili katika michuano hiyo.
Hata hivyo, uongozi umesema sababu za kufanya hivyo ni kutokana na weachezaji wa timu A kuwa katika mandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 21, 2012.
Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliokwenda Visiwani Zanzibar chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro ni pamoja na Idrisa Rashid, Said Mohamed, Salum Telela, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Rashid Gumbo, Omega Seme, Jerry Tegete na Zubery Ubwa

Comments