YANGA WAINYIMA USINGIZI ZAMALEK



Na Dina Ismail
WAPINZANI wa klabu ya Yanga katika ligi ya mabingwa barani Afrika Zamalek ya Misri wamezidi kuingiwa na mchecheto dhidi ya wapinzani wao hao siku ikiwa ni wiki chache kabla ya kuvaana.

Timu hizo zitacheza mechi ya awali kati ya Februiari 17 na 19 jijini Dar es Salaam kabl ya kurudiana Machi 2 na 4 huko Cairo, Misri.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Misri Zamalek wamekuwa wakihaha kwa namna moja aman nyingine ili kupata taarifa zaidi dhidi ya wapinzani wao hao.

Hofu ya Zamalek inatokana na kuvuliwa ubingwa na ligi hiyo mwaka 2003 na mahasimu wa Yanga, Simba, hali inayowafanya kujiimarisha zaidi kabla ya kuvaana.

Taarifa kutoka Misri zinaeleza kuwa kwa sasa wamekuwa wakihitaji kila aina ya taarifa zinazoihusu klabu ya Yanga ili kuweza kuzifanyia kazi.

“Hawa watu kwa kweli wanatapatatapa sana wameshaagiza mawakala wao huko kuhakikisha wanawatumia taarifa zote zinazoiuhusu Yanga, iwe mechi ama ama wachezaji,”Alisema mtoa habari huyo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wao wakuwafahamu vema wapinzani wao hao ambapo hivi karibuni kulikuwepo na taarifa za kuwepo kwa dau la kununua mikanda ya mechi za YAngha ili ikafanyiwe kazi.

Wamisri hao kwa sasa wapo katika maandalizi dhidi ya mechi hiyo huku wakizuia mashabiki kuhudhuria mazoezi ama mechi zao.

Comments