YANGA KUPIGA PANGA WACHEZAJI

KUTOKANA na hali ya ukata inayoikabali klabu ya soka ya Yanga, uongozi wa Yanga ume kusudia kupunguza wachezaji wachezaji wake hadi kubaki na 25 tu.
Hatua hiyo inafikia hali ya ukata inayoukabali klabu hiyo ambayo imekuwa ikifanya maandalizi ya kusuasua huku ikiwa inakabiliwa na mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zamalek ya Misri.
Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amesema leo kwamba kiasi cha fedha kinachoingia katika klabu hiyo hakiwezeshi kutimiza mahitaji ya walengwa ambao ni wachezaji, benchi la ufundi na masuala ya utendaji.
Nchunga alisema kutokana na hatua hiyo, wachezaji hawana budi kutimiza malengo yao yaliyowapeleka klabuni hapo badala ya kukaa na kuendesha migomo ya chini chini kwani kwa kwenda kinyume na sheria za klabu ni wazi panga litawakuta.

Comments