UTENDAJI WA TENGA WAIVUTIA VODACOM

WADHAMINI wa ligi kuu soka Tanzania Bara, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wamemmwagia sifa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodgar Tenga kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka hali inayowafanya wafikirie kuingia mkataba mwingine wa udhamini wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Mkataba wa Vodacom na TFF unafika tamati mwezi Septemba mwaka huu, ambapo tangu walipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2007 na kufanikiwa kwa vitendo hivyo kuiweka nchi pazuri, katika sekta ya michezo na hasa mpira wa miguu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa kitengo cha udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema kuwa katika udhamini huo, Vodacom wametumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 kwa ligi nzima ikiwa ni mpango wenye dira ya kuhakikisha kwamba soka linapiga hatua.

Alisema kwamba mkataba wao mpya watakaoingia mwaka huu ni matunda ya uongozi bora wa Tenga na timu yake hivyo anaamini utaweza kuinua kiwango cha soka kupitia ligi kuu Bara inayotarajiwa kuanza Januari 21 katika viwanja mbalimbali nchini.

Timu zinazotarajiwa kushiriki katika mzunguko huo wa lala salama ni pamoja na Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Mtibwa Sugar, JKT Oljoro, Coastal Union ya Tanga, Villa Squad, African Lyon, JKT ruvu, Ruvu Shooting, Kagera Sugar, Toto African ya Mwanza, Moro United.

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHJanuary 18, 2012 at 6:50 AM

    MICHAEL UMEISIKIA HIYO,WADHAMINI BADO WANAMKUBALI TENGA AMBAE WEWE UNAOTA KUPAMBANA NAE WAKATI WEWE UNAKOSA SIFA YA UADILIFU MWENZAKO WENYE PESA WANAMUAMINI,HIYO NI CHALLENGE KWAKO KAMA BADO UNA NIA YA KUGOMBEA URAIS TFF

    ReplyDelete

Post a Comment