UBABE WA BARCA KWA REAL WAELEKEA UKINGONII

UBABE wa Barcelona kwa Real Madrid sasa unaelekea ukingoni na hilo linadhihirishwa na matokeo ya mchezo baina ya timu hizo jana kwenye Uwanja wa Camp Nou. Timu hizo zimetoka sare ya 2-2 katika Robo Fainali ya pilib ya Kombe la Mfalme, maana yake kwa matokeo ya mchezo wa kwanza Santiago Bernabeu, Barca kushinda 2-1, Real imetolewa kwa jumla ya mabao 4-3. Imetolewa kiume. Kwa sababu pia Real walilazimika kucheza 10, baada ta Sergioa Ramos kulimwa kadi nyekundu na kocha Jose Mourinho amelalamikia hujuma kwenye mechi hiyo.   
Sergio Ramos kulia akipewa kadi nyekundu.
Lionel Messi akimkokota Xavi Alonso.
Cristiano Ronaldo akilalamikia 'hujuma'

Comments