TWIGA STARS KUAGWA KESHO

NAIBU Waziri wa Jinsia na Maendeleo ya Jamii Ummy Mwalim kesho  anatarajiwa kuikabidhi bendera ya Taifa timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambayo inatarajiwa kuondoka usiku  kwenda nchini Nambia katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayopigwa huko Januari 14.
Hafla ya kukabidhi bendera hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ofisi za Shirikisho la soka Tanzania (TFF) saa nane mchana ambapo timu hiyo itaondoka usiku wa kesho kuelekea Afrika Kusini na baadaye Windhoek, Namibia.

Comments