SIMBA YATAHADHARISHA WAAMUZI VPL

KLABU ya soka ya Simba imetoa tahadhari kwa  waamuzi watakaochezesha mzunguko wa pili wa ligi kuu bara kuwa makini na vitendo vya utovu wa nidhamu pamoja na kuumizwa wanavyofanyiwa wachezaji wao na wachezaji wa timu pinzani.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wameaamua kutoa tahadhari mapema kwani katika mzunguko wa kwanza  wachezaji wao wengi waliumizwa kwa makusudi lakini waamuzi walishindwa kutoa adhabu ama onyo kwa walioshiriki kufanya hivyo.
Alisema kumeibuka tabia ya kuumiza wachezaji nyota na wale wa kigeni kwa lengo la kuwa kufanya hivyo kutachangia kushusha ama kuhuisha viwango vyao sambamba na kuizorotesha timu kwa namna moja ama nyingine.
Kamwaga alisema katika mzunguko wa kwanza wachezaji wao wakiwemo Felix Sunzu, Gervais Kago waliumizwa kwa makusudi na mwamuzi aliyekuwepo hakutoa adhabu yoyote.

Comments