SIMBA YAICHOMOLEA SOFAPAKA

VINARA wa ligi kuu bara, timu ya soka ya Simba imechomoa kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi yake na Sofapaka ya Kenya iliyokuwa ipigwe kesho kwenye dimba lka Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba benchi la ufundi limeamua kuachana na mechi hiyo kutokana na kuhofia kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chake hali itakayopelekea timu hiyo kushindwa kufanya maandalizi yake ya mechi za ligi kuu pamoja na kombe la Shirikisho.
Kamwaga alisema mpaka sasa wachezaji watatu wa timu hiyo Haruna Moshi 'Boban', Felix Sunzu na Ulimboka Mwakingwe.
Simba kwa sasa imejichimbia katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHJanuary 18, 2012 at 6:37 AM

    Heee! simba sasa hamtaki kucheza mpira?!!!basi bora iwe club ya karata na draft kama hivyo kwani leseni inaruhusu,maana simba imesajiliwa kama sports club,hivyo soka si lazima sana kama mnaona ngumu,michezo iko kibao...

    mdau wa bomba la uhuru,Revere,masachusetts,USA

    ReplyDelete

Post a Comment