SIMBA YAICHOMOLEA SOFAPAKA NA KUILETA TUSKER

VINARA wa ligi kuu bara timu ya Simba imechomoa mechi baina yake na Sofapaka ya Kenya badala yake sasa itacheza na Tusker ya Kenya jumapili hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es SAlaam.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' amesem kwamba hawafahamu uwepo wa mchezo baina yao na Sofapaka, na ndiyo maana wameialika Tusker ambayo itawasili leo.
Mapema wiki hii taasisi moja inayokuza na kuendeleza soka la Vijana ilitangaza kuileta Sofapaka kwa ajili ya kucheza na timu za Simba na Yanga Januari 14 na 15.

Comments