SIMBA WAOMBOLEZA KIFO CHA MBUNGE JEREMIAH SUMARI


 MAREHEMU JEREMIAH SUMARI
RAIS Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM) Jeremiah Sumari leo katika viwanja vya Karimjee.

KLABU ya soka ya Simba imetuma salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  kufuatia kifo cha mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari na kusema Simba imepokea kwa mshtuko taarifa za kifo hicho kwani marehemu alikuwa ni mmoja ya wadau walikuwa wakiifuatilia kwa karibu timu ya Simba.
“Tunaungana na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha mbunge Sumari ambaye alikuwa ni mtu wa karibu katika klabu ya Simba, tunamuomba mwenyezimungu aipumzishe roho yake pema peponi, Amin”, Alisema Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHJanuary 21, 2012 at 11:15 PM

    wanyama bana msije mkatuambia na huyu alikua mnyama .....


    mdau wa bomba,Revere masachussetts,us

    ReplyDelete

Post a Comment