SIMBA SC WAMLILIA REGIA MTEMA

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba  umtuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Regia Mtema (pichani).

Ofisa Habari wa Simba Ezeckiel Kwamwaga, amesema kwamba uongozi umepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mtema na hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa bado ni kijana hivyo mchango wake bado ulihitajika.

Alisema kuwa marehemu ambaye enzi za uhai wake alikuwa Mwanachama wa klabu ya Simba, pigo lake si kwa familia tu na Watanzania, bali ni kwa Wanasimba ambao wataendelea kukumbuka mchango wake.

“Marehemu Regia alikuwa mwanachama halali wa Simba Sports Club, kama mtakunbuka baba yake mkubwa Privatus Mtema aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba,hivyo sisi kama Simba tunamuombea mwenyezi mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi,”Amina

Mtema ambaye alikumbwa na mauti hayo jumamosi iliyopita katika eneo la Ruvu mkoani Pwani, anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Ifakara mkoani Morogoro.

Comments