SHEREHE ZA CCM ZABADILI RATIBA VPL


Mechi kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ichezwe Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza haitakuwepo, na sasa itapangiwa tarehe nyingine.
 
Juzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipokea barua kutoka kwa wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba ikieleza kuwa Februari 5 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo hautaweza kutumika kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.
 
 
Powered by Sorecson : Creation de site internet

Comments