REDIO RUKSA KURUSHA VPL,TV BADO HAKIJAELEWEKA


SHIRIIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mpaka sasa hakuna kituo cha televisheni ambacho kimeomba na kushinda tenda ya kuonesha moja kwa moja (live) mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa upande wa vituo vya redio, vyote vimepewa haki ya kutangaza moja kwa moja mechi za ligi hiyo kwa masharti yafuatayo;
 
Kuitambulisha ligi hiyo kwa jina lake (Ligi Kuu ya Vodacom) wakati wa matangazo hayo ya moja kwa moja, na pia kuweka matangazo ya mdhamini (Vodacom) wakati wakitangaza mechi husika. Hata hivyo, vituo vya redio bado vinaruhusiwa kuendelea kutafuta/kutumia matangazo ya wadhamini wao, lakini ambao si washindani wa kibiashara wa Vodacom.
 

Comments