PAPIC ACHARUKA TENA YANGA

KOCHA mkuu wa Yanga Kostadin Papic ameibuka na kusema kuwa hali ndani ya klabu hiyo si shwari na wachezaji wametangaza kususia mazoezi iwapo hawataliwa stahiki zao.
Hii ni mara ya pili kwa siku za hivi karibuni kwa kocha huyo kupasia jipu ndani ya klabu hiyo kuhusiana na masuala mbalimbali na hasa hali ya ukata ambayo imekuwa ikiikabili klabu hiyo.
Papic amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi mara kwa mara ili kupata ufumbuzi juu ya suala hilo lakini hakuna hata kiongozi mmoja aliyeonekana kuchululia umuhimu suala hilo.
Alisema hali hiyo ni ngumu katika kipindi hichi ambacho timu inakabiliwa na maandalizi ya michezo muhimu iliwemo klabu bingwa ya Afrika  na mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Akienda mbali zaidi, Papic alisema hali hiyo ndiyo ilipelekea timu yao kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Comments