OKWI ASAMEHEWA, COSTA AKATWA MSHAHARA


Na Dina Ismail

WAKATI Simba ukifuta na adhabu iliyopanga kumpa mshambuliaji wake wa kimataifa Emmanuel Okwi, uongozi wa klabu hiyo umemrejesha kundini beki wake aliyekuwa akitumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana, Victor Costa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, mmoja ya viongozi wa Simba alisema kuwa wameaona si jambo la busara kumuadhibu Okwi ambaye alitimkia kwao mwishoni mwa mwaka jana na kushindwa kuripoti kama alivyotakiwa kutokana na kubaini kuwa mchezaji huyo alikuwa anakabiliwa na tatizo la pasi yake ya kusafiria.

Alisema kuwa baada ya kutokuwepo mawasiliano baina yao na nyota huyo walituma mmoja ya viongozi kwenda Uganda na kwa bahati nzuri alikuta mchezaji huyo yupo katika jitihada za kusaka hati nyingine na hivyo kumsaidia kupata hati mpya.

“Kweli tuliahidi kumuadhibu Okwi, lakini baada ya kutuma mjumbe kule Uganda tulikuta kweli anashughulikia hati ya kusafiria na mjumbe huyo alilisimia suala hiyo na ikapatina ndipo alirejea naye nchini sasa hapo tunaona ni ngumu kidogo kutoa adhabu kwa kitu kilicho wazi kama hicho,”Alisema.

Kuhusiana na Costa ambaye alikumbana na adhabu hiyo baada ya kufanya utovu wa nidhamu wakati timu ilipokuwa Visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, alisema pamoja na kurejeshwa kundini mchezaji huyo atakatwa nusu mshahara wake wa mwezi Januari.

Alisema mchezaji huyo ametakiwa kuungana leo na wenzake waliopo kambini katika hoteli ya Bamba iliyopo KIgamboni, jijini Dar es Salaam wakijiandaa na michezo ya ligi kuu soka Tanzania Bara pamoja na kombe la Shirikisho ambapo watacheza na KIyovu ya Rwanda mwezi ujao.

“Pamoja na hilo pia tumempa onyo kali mchezaji huyo iwapo atarudia tena kufanya kosa jingine basi uongozi hautasita kumchukulia hatua kali za kinidhamu,”Aliongeza kiongozi nhuyo.

Comments