Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi
nne. Moro United itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu,
Turiani.
Nayo Toto Africans itakuwa
mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani na Villa Squad
itapambana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es
Salaam.
Januari 22 mwaka huu JKT Ruvu
na Polisi Dodoma zitapepetana Uwanja wa Azam Chamazi wakati Januari 22 mwaka huu
Dar es Salaam itakuwa na mechi mbili; African Lyon na Azam (Uwanja wa Azam
Chamazi) na Simba na Coastal Union (Uwanja wa Taifa).
Ratiba kwa ajili ya waamuzi
na makamishna kwa mechi 35 za mwanzo tayari imeshatoka. Waamuzi wa kati 16
wameteuliwa kuchezesha mechi hizo huku watatu wakiwa wenye beji za Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Makamishna ni 28 huku watathmini wa waamuzi
(referees assessors) wakiwa kwenye mechi tano. Watathmini hao ni Charles Mchau,
Soud Abdi, Emmanuel Chaula, Army Sentimea na Joseph Mapunda.
UWE FASTA KUTUWEKEA MATOKEO,TENA YOTE SIO YA WANYAMA AU YANGA TU...SIE WENGINE TUKO MBALI NA TUNAKUTEGEMEA WEWE ZAIDI KWENYE MASUALA YA SOKA!
ReplyDeleteMDAU WA YANGA BOMBA,REVERE,MASSACHUSSETTS