Mwape (kulia) akiwa na mtoto wa Mamapipiro (Prince Akbar AKA Ince), kushoto ni kipa wa Yanga, Yaw Berko.

Na Dina Ismail
WAKATI uongozi wa klabu ya soka ya Yanga ukidai mshambuliaji wake wa Kimataifa Mzambia Davies Musonda Mwape yu Mgonjwa, nyota huyo ameibuka na kudai yupo fiti  kwa asilimia 100 ila hajisiki kucheza.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kutoka kutoka kwao zambia jana, Mwape alisema hana majeruhi wala haumwi ila kisaikolojia hayupo fiti kwa asilimia 100
Mwape ambaye hakuwa tayari kusema lini atarejea amekuwa tegemo katika safu ya ushambuliaji tangu ajiunge na timu hiyo msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Orlando Poirates ndiye aliyefunga bao la pekee la ushindi katika mechi ya watani Simba oktoba 31, 2011 kwenye Uwanja wa Taifa.
Lakini tangu wamepewa likizo baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza hajajiunga na timu yake huku uongozi ukidai anumwa nyama za paja.
Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema jana kwamba Mwape bado anaumwa nyama za paja na yupo kwao Zambia akiendelea ku7jiuguza.
“Mimi ninachofahamu Mwape ni mgonjwa na ametakiwa kujitibia majeruhi yake kutokana na ukweli kwamb a amekuwa akiandamwa na matatizo haya kila mara,”Alisema.
Yanga tayari ipo kambini ikijandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu bara  na ligi ya mabingwa barani Afrika, michuano ambayo wataanza na Zamalek ya Misri mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa sasa baadhi ya wachezaji wa Yanga wapo Zanzibar katika kombe la Mapinduzi na wengine wapo jijini Dar es Salaam wakiendelea na mazoezi katika Uwanja wa Loyoila.
Kutofautina kwa kauli za Yanga na  Mwape kunaashiria kwamba kuna kitu kimejificha katika baina ya pande hizo mbili ambapo hakuna upande uliokuwa tayari kukifichua.
mwisho

Comments