MWALALA,MGUNDA WAVAA VIATU VYA JULIO

KUFUATIA kutimkia Uarabuni kwa kocha mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Jamhuri Kihwelo 'Julio' uongozi wa timu hiyo umeamua kuwapa jukumu la kukinoa kikosi hicho, JUma Mgunda na Ben Mwalala, imefahamika.
Ofisa habari wa Coastal Union Eddo Kumwembe amesema jana kwamba kwa sasa timu hiyo inayojiandaa na mzunguiko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara, ambapo Mwalala alipendekezwa na Julio kuwa msaidizi wa Mgunda ambaye alikuwa akimsaidia Julio.

Comments