MUSTAFA HASSANALI AANDAA ONYESHO LA KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO


MBUNIFU wa mavazi nchini Mustafa Hassanali na meya wa Ilala Jerry Slaa wameandaa onyesho maalum la mavazi kwa ajili ya kuchangia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2011 linatarajiwa kufanyika Januari 12 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Hassanali alisema kuwa mavazi yatakayoonyeshwa ni yale aliyoyazindua mwishoni mwa mwaka 2011 katika nchi za Afrika Kusini, Angola, Niger na Sweden.
Alisema kupitia maonyesho hayo kutafanyika mnada wa mavazi hayo ambapo asilimia 10 ya mapato yatapelekwa katika mfuko maalum wa kuwasaidia waathirika hao.

Comments