MNYIKA MGENI RASMI FAINALI ZA KOMBE LA KINESI KESHO

MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika (pichani)lkesho  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali za soka za kuwania kombe la Kinesi ukizikutanisha timu za Simba B na Friends Rangers kwenye dimba la Kinesi, jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba timu yake imejipanga vema kuhakikisha inashinda mchezo huo ambao utakuwa wa kihistoria kwa timu hiyo.
“Kama mnavyofahamu timu yetu haijawahi kufika fainali tangu kuanzishwa kwa michuano hiii karibu miaka 20 hivyo kufika fainali tu ni jambo la kihistoria…hivyo nawaomba wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia,”Alisema.

Comments