MILIONI 10 ZA PINDA KWA STARS ZAKABIDHIWA MAHALA PAKE

WAZIRI Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari amekabidhi sh. milioni 10 kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwa ni ahadi yake aliyotoa kwa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikiwa ni motisha kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mechi yao na Chad iliyochezwa Novemba Mosi mwaka jana jijini N’Djamena.

Pinda alitoa ahadi hiyo siku chache kabla ya Stars kuwakabili Chad katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunai kwa kanda ya Afrika ambapo Stars ilishinda ugenini mabao 2-1 hivyo kuwatoa Chad kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema kwamba BMT iliwataka watoe mchanganuo wa fedha hizo na TFF ikampa jukumu hiko Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso ambaye ameshaanda orodha ya wachezaji wanaostahili kunufaika na ahadi hiyo.

Alisema wameshapokea mchanganuo na hivyo wanatarajiwa kuiwasilishi BMT ili kuweza kupatiwa fedha hiyo kwa ajili ya mgawo kwa wahusika hivyo kuondoa wasiwasi uliojitokeza hivi karibuni kuhisana na fedha hizo.

“Tunamshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa ahadi hiyo, kwani Taifa Stars ilifanikiwa kushinda mechi hiyo ya ugenini ambao bila shaka ulichagizwa na ahadi hiyo hivyo tunaamini na wadau wengine watakuwa wakifanya hivyo,”Alisema.

Comments