MAMBO YAMEIVA JANGWANI, YANGA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI ITAKAYO

KLABU ya soka ya Yanga leo imesaini mkataba na Kampuni ya National Estate & Designing Consultancy Company (NEDCO Ltd) kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la kisasa pamoja na Uwanja wa Kaunda kwenye mtaa wa Mafia, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ya utiaji saini mkataba baina ya pande hizo mbili imefanyika katika  Hoteli ya Courtyard baada ya makubaliano ya pande zote kufuatia  namna mchakato wa tathmini ya awali ya ujenzi huo ulivyokwenda
vizuri.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Yanga, LLoyd Nchunga mradi huo unakadiriwa kuwa na thamani kati ya bilioni 4 hadi 5 na hivyo kutengeneza ajira za muda na hata za kudumu hata utakapokamilika.
"Ni matuaini yangu kuwa sehemu kubwa ya vifaa vya ujenzi vitatoka hapa nchini na wataalamu wa ujenzi uliopo, kwa faida ya uchumi na taifa letu kwa ujumla,"Alisema Nchunga.
Aidha, mradi huo utahusisha pia ujenzi wa Uwanja wa kisasa ambao utaweza kubeba watu 12,000 hadi 15,000., maduka 50, ofisi 20, hosteli itakayobeba wanamichezo 30, Parking itakayoweza kuchukua magari 200, baiskeli 1000, cliniki ya kuhudumia wanamichezo, Mafia Complex na kuboresha Swiming Pool.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHJanuary 21, 2012 at 5:34 AM

    HAYA NDIO MAMBO YATAKAYOMUACHIA LOYD NCHUNGA LEGACY YA KUTUKUKA KULIKO WENYEVITI WOTE WALIOWAHI KUPITA HAPO UKIMUACHA MZEE WETU MANGARA TABU,NCHUNGA AKOMAE NA HII ITAMTOA NA YANGA HAITOKUJA KUMSAHAU,AACHANE NA WAPIGA DOMO KINA DEVI MOSHA NA VIMILIONI KUMI VYAO!KWANZA SO FAR UWANJANI NCHUNGA AMESHAPATA REKODI YA KUJUJIVUNIA NA YA KUKUMBUKWA YA UBINGWA KAGAME CUP!AWAMALIZE WAPINZANI WAKE WALIOKUWA WANADAI HAJUI MPIRA NI KITU CHA UJENZI KWISHNEY!

    MDAU WA BOMBA REVERE,MASACHISSETTS,US

    ReplyDelete

Post a Comment