MALI, GHANA ZAPETA AFCON



FRANCEVILLE, Gabon
NAHODHA wa Ghana, John Mensah aliipigia timu yake bao kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu, Black Stars wakishinda 1-0 dhidi ya Botswana katika mechi ya Kundi D ya Fainali za Kombe la Mataifa la Afrika.
Mensah alipiga bao hilo kutokana na kona dakika ya 25 kwenye Uwanja wa Stade de Franceville, ambao ulikuwa umekusanya nusu ya idadi ya watu wa kuujaza.
Lakini Mensah alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 66 baada ya kumchezea rafu Jerome Ramatlhakwane akiwa katika eneo la hatari na kuwaacha mabingwa hao mara nne Afrika wakihenyeshwa katika mchezo waliotarajiwa kushinda kiulaini.
Kikosi cha Ghana kilikuwa: Adam Kwarasey, Asamoah Gyan, John Pantsil, John Mensah (sent off, 66), Anthony Annan, Samuel Inkoom, Emmanuel Agyemang Badu, Andre Ayew/Mohamed Abu dk 88, Sulley Muntari/Jonathan Mensah dk 72, Jordan Ayew/Masahudu Alhassan, dk 53 na John Boye.
Botswana: Modiri Marumo, Ndiyapo Letsholathebe, Mosimanegape Ramohibidu, Mompati Thuma, Ofentse Nato, Phenyo Mongala, Jerome Ramatlhakwane, Moemedi Moatlhaping, Patrick Motsepe/Mogakolodi Ngele dk 60, Mogogi Gabonamong, Tshepo Motlhabankwe.
Katika mchezo wa pili, bao pekee la Bakaye Traore liliipa ushindi wa 1-0 Mali dhidi ya Guinea. Kikosi cha Mali kilikuwa: Soumaila Diakite, Adama Tamboura, Cedric Kante (capt), A. Traore, Diabate, Modibo Maiga, Seydou Keita, D. Diakite, B. Traore, Samba Diakite na N'diaye
Guinea: Yattara, Feindouno, D. Bah, B. Balde, Zayatte (capt), I. Traore, Bangoura, L. Bah, Diallo, A. Bangoura na H. Balde. 

Comments