MADARAKA NYERERE NDANI CHEKA V NYILAWILA

Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Godfrey Madaraka Nyerere ataiwakilisha TPBC kwenye pambano kati ya Francis Cheka na Karama Nyilawila litakalofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Morogoro siku ya jumamosi tarehe 28 mwezi huu.
Madaraka ambaye ni Makamu wa Rais wa TPBC anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala atakuwa meza kuu pamoja na mgeni rasmi wa mpambano huo. Promota wa mpambano huu ni Philemon Kyando wa Kyando Boxing Promotion.
Pambano la Ngumi kati ya Francis Cheka na Karama Nyilawila litakuwa la raundi 10 ambapo kila raundi itakuwa ni ya dakika tatu. Mpambano huu utasimamiwa na Injinia wa ndege, Nemes Kavishe kama ambaye atakuwa ndiye refarii wa pambano.
Madaka anaondoka Butiama kwa ndege siku ya Ijumaa tarehe 27 kuelekea Dar-Es-Salaam ambapo kesho yake asubuhi ataelekea jijini Morogoro tayari kuiwakilsha TPBC kwenye mpambanpo huo wa mafahali wawili!
Tarehe 12 Februari kutakuwa na mpambano mwingine kati ya Khamisi Mwakinyo na Sais Mundi utakaosimamiwa na TPBC jijini Tanga katika ukumbi wa Ridoch.
Aidha, tarehe 7 March kutakuwa na mpambano mwingine mjini Moshi Hugo Hotel Ltd utakaosimamiwa na TPBC ambako bodia wa kimataifa Pascal Bruno atapambana na bondia James Onyango toka Kenya.
Pia, siku ya Mei mosi TPBC imeidhinisha pambano jijini Arusha kati ya bondia Rashid Matumla na Francis Cheka katika uwanja wa Sheik Amri Ebeid.
Huu ni utaratibu mpya wa TPBC kuzisambaza ngumi mikoani ili kutoa nafasi kwa vijana wengi wenye vipaji kujionyesha.
Onesmo A.M.Ngowi
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
Technology House, 35-38 Ghalla Road
P.O BOX 1106, Moshi - Tanzania
Tel: + 255-2727-53434 (Office)
Tel: + 255-2727-55118 (Residence)
Cell: + 255-754-360828
Fax: + 255-2727-54743
E-mail:
ngowio@yahoo.com
ibfafrica@yahoo.com
Webs: www.ibf-usba-boxing.com www.commboxing.com

Comments