LICHA YA NJAA YANGA,PAPIC ANAKWEA PIPA KILA SIKU KWENDA ZANZIBAR

WAKATI wiki iliyopita kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic alidai kuwepo na hali mbaya ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kiasi cha kutishia maandalizi ya timu hiyo, wiki hii Mserbia huyo amekuwa akikwea pipa kutoka Dar na kwenda Zanzibar ili kukishuhudia kikosi chake kinachoshiriki kombe la Mapinduzi.

Hatua hiyo inafuatia kikosi cha pili cha timu hiyo na baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kushiriki katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar kikiwa chini ya kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro huku Papic akibaki Dar kukinoa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mzunguko wa pilki wa ligi kuu na ligi ya mabingwa ambapoi Yanga itaanza kwa kucheza na Zamalek ya Misri.
Hata hivyo Papic amelazimika kupanda ndege kwenda Zanzibar ili kukishuhudia kikosi hicho pindi kinaposhuka uwanbjani na kisha kurejea Dar kuendelea na majukumu yake.
Si jambo la ajabu kwa Papic kwenda Zenji na kurudi Dar lakini kinachoshangaza ni hali ya ukata inayoikabili timu hiyo ambayo mwenyewe aliitangaza na kuendelea kusisitiza lakini mwisho wa siku ukata huo unaonekanma ni kwa maandalizi ya timu na mishahara ya wachezaji na si kwa  fedha zake za posho.

Comments

  1. Sasa yana kuhusu nini...kama anajilipia mwenyewe...acha kufuatilia ya wenzako pungunza unene huo wewe unadhani ni sifa hiyo.

    ReplyDelete
  2. ulikuwa unataka akuchukue na wewe mwende wote?

    ReplyDelete

Post a Comment