FEDHA ZA PINDA ZAWAFIKIA WACHEZAJI

HATIMAYE wachezaji wa timu ya soka ya Taifa na benchi la ufundi la timu hiyo jana wamekabidhiwa kitita chao cha shilingi milioni kumi zilizotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama motisha kwa timu hiyo iwapo ingeitoa Chad katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia Kanda ya Afrika.

Pinda alitoa ahadi hiyo siku chache kabla ya Stars kurejeana na Chad Novemba Mosi huko N’Djamena, Chad ambapo Stars ilishinda mabao 2-1 na hivyo kuisukumizia nje kwenye michuano hiyo.Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.



Comments